SIMULIZI YA KOSA LANGU SEHEMU YA TATU

SIMULIZI YA KOSA LANGU SEHEMU YA TATU

SIMULIZI YA KOSA LANGU SEHEMU YA TATU

Baada ya kumuhifadhi Marehemu kwenye makazi yake ya milele, watu walitawanyika pale nyumbani na kuwaacha akina Joyce wakiwa na simanzi na wakati huo waliishi kwa kumtegemea Mzee Ngonyani na mke wake,maisha yaliendelea huku baadhi ya watu wakitoa michango yao kwa ajili ya matibabu ya Mama Joyce ambaye alikuwa amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Yule rafiki yake na marehemu mzee Ndesanjo alirudi Dar es salaam baada ya mazishi ya mke wake kule Morogoro na muda wote alikuwa hajui nini kimempata rafiki yake kipenzi kwani hata marafiki zake walimficha kwasababu naye pia alikuwa katika matatizo ya kufiwa na mke wake, aliporudi Dar es salaam alielekea nyumbani kwa marehemu ili kumjulia hali alipofika alimkuta Mama Ngonyani akiwa pamoja na Joyce wakiwa wanajiandaa kwenda hospitali kumuona mgonjwa Joyce alikuwa akimfahamu rafiki wa baba yake ambaye alikuwa akifahamika kwa jina la Beni basi alipomuona akaanza kumfuata huku akilia kwa uchungu “Baba mdogo Baba mdogo, ulikuwa wapi Baba yangu amefariki na mama anaumwa sana” Mzee Beni alimuangalia Joyce kwa makini kisha akasema “etii!Mzee Ndesanjo amefariki haiwezekani jamani nini kilitokea,siamini mimi haya maneno” alizungumza huku akiwa amemshika mkono Joyce aliyekuwa analia kwa uchungu.



Mama Ngonyani akamsimulia kila kitu kuhusu ajali waliyoipata marehemu Mzee Ndesanjo na mkewe wakati wakielekea msibani Morogoro, Mzee Ben aliinama kwa uchungu na kuanza kulia kwa kumpoteza rafiki yake,Baadaye waliondoka pamoja hadi hospitalini kwenda kumtizama Mama Joyce anaendelaje walipofika walimkuta amezinduka lakini alikuwa haongei chochote muda wote alikuwa kimya na alimshangaa kila aliyekuwa anamuona Joyce aliyekuwa karibu na mama yake alimuita “mama, mama mimi mwanao Joyce ongea basi mama hata kidogo” alimuita bila mafanikio mama yake alibaki akimshangaa bila kusema chochote hali ile iliwatatiza sana Mzee Beni na Mama Ngonyani waliokuwa pale hospitalini iliwabidi waende kumuona Daktari ili waweze kufahamu zaidi, ndipo Daktari akawaeleza kuwa mgonjwa amepoteza kumbukumbu zote kwani katika hali aliyonayo hawezi kumkumbuka hata mtoto wake na pia kuna uwezekano hata kama akirudi katika hali yake basi atakuwa hana akili vizuri Mama Ngonyani kusikia hivyo alishtuka na kusema “Mungu wangu sasa itakuwaje ndiyo tumekwisha mpoteza mama Joyce, ina maana Daktari hakuna njia yoyote ya kumrudisha katika hali yake ya kawaida, tusaidie jamani” alizungumza mama Ngonyani huku machozi yakiwa yanamdondoka Daktari alimjibu akisema “Huwezekano hakuna kilichobaki ni Kumuomba Mungu amsaidie pia tunaweza kumruhusu kesho ili muweze kumuhudumia akiwa nyumbani”.



walibaki wanasikitika na kutafakari, baadaye ilibidi waondoke na kesho yake walirudi kwaajili ya kumchukua mama Joyce ambaye alikuwa haelewi chochote.Maisha yalianza kubadilika kwa mtoto Joyce aliyekuwa na Malengo ya kusoma na baadaye kuwa Mwanasheria hali ilizidi kuwa ngumu kwani Mama Joyce alikuwa akihitaji huduma wakati wote ilifikia kipindi familia ya Mzee Ngonyani ikaanza kuwatenga na hata waliokuwa marafiki waliwaacha wakitaabika wenyewe, Kutokana na hali kuwa mbaya Joyce aliamua kuacha masomo akiwa darasa la sita ili aweze kumsaidia mama yake pale nyumbani Mzee Ngonyani na Mkewe waliamua kuhama katika ile nyumba na tokea walipohama hawakuwahi kurudi hata siku moja kwenda kumsalimia mama Joyce, hali ilizidi kuwa mbaya Joyce na mdogo wake ilibidi wakati mwingine waende mitaani na kuomba msaada angalau wapate pesa ya kula pale nyumbani.



Siku moja Mama Joyce aliamka asubuhi kichwa kilikuwa kinamuuma sana hivyo alitakiwa apelekwe hospitali ambapo Joyce alikuwa hana chochote kwani alikuwa akitegemea biashara ya kuuza maandazi na pesa ilikuwa ni ndogo alihangaika sana bila kupata msaada wowote hatimaye Mama Joyce alifariki Dunia kutokana na kuumwa sana bila kupata matibabu, Aliwaacha Joyce na James ambao sasa walikuwa ni yatima maisha yalikuwa magumu hawakujua nini cha kufanya kwani hata nyumba waliyokuwa wakiishi walifukuzwa kutokana na kushindwa kulipa kodi, hivyo kujikuta wakirandaranda mitaani kutafuta kipato…… nini kitatokea huko mitaani na nini hatma yao usikose sehemu ya 4

No comments:

Post a Comment

WATOTO MAPACHA Sehemu ya ,,7

WATOTO MAPACHA Sehemu ya ,,7 Celena alienda shuleni kwao baada ya mama yake kupata nafuu , alipofika ,akashangaa kuitwa ofisini na kupewa ho...