KOSA LANGU SEHEMU YA PILI
Baada ya wasamaria kumkimbiza hospitalini Mama Joyce ambaye kwa wakati huo alikuwa hajitambui Askari Polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu wa Baba Joyce na kuupeleka chumba cha maiti hospitali ya Morogoro, gari lilikuwa limeharibika sana kutokana na ajali ilivyokuwa mbaya hivyo ulifanyka utaratibu wa kulisogeza hadi kituo cha polisi, wakiwa hospitalini Mama Joyce alikuwa hajitambui kabisa na hivyo Polisi waliamua kufanya utaratibu wa kufahamu ndugu ambao wangeweza kuwa naye karibu kwa wakati huo, mmoja wa mapolisi alimwambia mwenzake "sasa tutafanyaje kuwapata ndugu wa hawa watu kwani huyu mama hajitambui na mume wake amekwisha fariki inabidi tuwatafute ili waendelee na taratibu nyingine" mwenzake ambaye alikuwa naye akamjibu na kusema "inabidi tupekue namba za simu katika simu zao na kuweza kuwasilia na ndugu zao" basi moja kwa moja alichukua simu ambayo ilikuwa ni ya baba Joyce na kuangalia namba za watu mbalimbali akiwa anatizama nani wa kumpigiia simu alijaribu jina ambalo lilikuwa kwenye simu ambalo liliandikwa Mkurugenzi alipiga namba hiyo bila mafanikio na alijaribu namba kama tatu zote zilikuwa hazipatikani.
Ndipo wakaamua kuchukua simu ya mama Joyce na kuangalia namba nyingine katika simu hiyo kwa bahati nzuri walikuta namba ya Mke wa Ngonyani ambayo ilikuwa imeandikwa Mama ngonyani na kujaribu kuipiga simu iliita kwa mara ya kwanza bila kupokelewa hadi ikakata lakini waliendelea kujaribu hatimaye simu ilipokelewa,Mama Ngonyani ambaye ni jirani wa Mama Joyce aliyekuwa amekabidhiwa watoto alipokea ile simu akijua mke wa Ndesanjo ndiye aliyempigia na kusema "Habari mama joyce nilikuwa mbali na simu vipi mmekwishafika" yule askari aliyekuwa anasikiliza ile simu alinyamaza kimya kidogo na kusema "samahani mama unazungumza na askari polisi kutoka Morogoro" kabla hajaendelea Mama Ngonyani alimkatisha na kusema kwa mshangao "askari! kwani kuna nini tena mama Joyce yuko wapi?" aliuliza mama Ngonyani yule askari akamwambia usijali mama nilikuwa nataka kufahamu unamfahamu vipi Mama Joyce" kwa haraka Mama Ngonyani akajibu "Mama Joyce ni jirani yangu na pia ni rafiki yangu na wameenda Morogoro kwenye msiba sasa nashangaa kuzungumza na askari kupitia simu yake kwani kuna tatizo" alizungumza mama Ngonyani huku akitaka kufahamu nini kinaendelea ndipo yule askari akamwambia kile kilichotokea "Mama Joyce na mume wake wamepata ajali maeneo ya kidatu na hapa ninapozungumza nipo hospitali ya Morogoro nilikuwa naomba ungewajulisha ndugu zake ili waje haraka" alizungumza yule askari lakini hakumwambia kama baba Joyce alikuwa amefariki.
kwa mshtuko mama Ngonyani akasema "Ajali? Mungu wangu jamani, kwahiyo wanaendeleaje sasa ndugu zake akinanani mimi ninachojua hawana ndugu zaidi ya watoto wao wawili Joyce na James ambao wapo hapa nyumbani na ni watoto wadogo sijui nifanyeje jamani" alizungumza maneno mengi kana kwamba mtu aliyechanganyikiwa kumbe masikini Mzee Ndesanjo na mke wake walikuwa hawana ndugu zaidi ya watoto wao yule askari alimsisitiza mama Joyce afike hospitali kwani kulikuwa hakuna mtu wa kumuhudumia mama Joyce basi Mama Ngonyani alimjulisha mumewe na haraka walijiandaa kwa safari ya Morogoro huku wakiwaacha Joyce na James bila kuwajulisha kile kilichotokea walipofika haospitalini ndipo walipogundua kuwa Baba Joyce alikuwa amefariki na hali ya mama Joyce ilikuwa mbaya sana walionana na daktari ambaye aliwaeleza iwapo mama Joyce akizinduka kuna uwezekano asikumbuke chochote kilichotokea kwani alikuwa ameumia sana maeneo ya kichwani maneno hayo yaliwasikitisha sana Mama Ngonyani na mume wake ambao waliamua kufanya utaratibu wa mazishi wakati huo Mama Joyce akiwa hajitambui walimuhamishia hospitali ya Muhimbili Dar es salaam kuendelea na matibabu na huko nyumbani mazishi yalifanyika vilio na simanzi vilitawala watoto walilia sana kwa uchungu wakati huo na hata kupoteza fahamu huku wakiwa hawajui ni hatma ya mama yao mzazi hapo ndipo maisha ya Joyce na mdogo wake yalianza kubadilika nini kitaendelea usikose sehemu ya tatu............

No comments:
Post a Comment