
Siku ya Ajali – Mei 21, 1996 Katika safari yake ya mwisho, MV Bukoba ilikuwa imebeba idadi kubwa ya abiria na mizigo kupita kiasi. Ingawa uwezo wake wa kubeba abiria ulikadiriwa kuwa watu 430, inadaiwa kuwa siku hiyo ilibeba zaidi ya watu 1,200, huku mizigo ikiwa na uzito wa zaidi ya tani 200. Meli ilizama ikiwa imebakisha umbali wa maili moja na nusu kutoka Bandari ya Mwanza Kaskazini, hali iliyowapa abiria matumaini kuwa walikuwa wamekaribia kufika salama. Ilipinduka karibu na ufukwe wa Shule ya Sekondari ya Bwiru, ambapo baadaye ilijengwa mnara wa kumbukumbu ya ajali hiyo. Watu waliokuwa ndani ya
No comments:
Post a Comment