
PENZI LA MHALIFU 42 Nilikuwa kwenye wakati mgumu kwa wakati huo kwani nilikuwa sitaki kabisa kuwa na mwanaume mwenye watoto wa nje ya ndoa. Upande wa chumbani Cyborg baada ya kuona nimechelewa kurudi chumbani uvumilivu ulimshinda, aliamua kuvaa nguo zake na kutoka chumbani. Alimkuta mfanyakazi na alikutana na taarifa kuhusu mtoto aliyekuja nae huku ikisemekana ni mtoto wake. Cyborg alimchukua mtoto na kujaribu kumwangalia kama watakuwa wanafanana. Baada ya kumuangalia Cyborg aliongea. "Wewe huyu sio mtoto wangu, mimi watoto wangu nawajua" "Ni wako kaka, wewe ndiye baba yake naomba uamini hilo" mfanyakazi wangu wa zamani aliongea na mimi mda huo
No comments:
Post a Comment