
PENZI LA MHALIFU 24 Sikujua alikuwa na mpango gani hivyo Cyborg aliondoka na kwenda kufanya kazi ya kuhubiri. Baada ya masaa kadhaa kupita Cyborg alikuja nyumbani akiwa na mfuko uliokuwa na sadaka na baadae alizimwaga kwenye meza iliyokuwa sebleni kwetu. "Leo nimehubiri sana sijui ata upako ulitokea wapi" Cyborg aliongea huku akifungua vishikizo vya shati lake. "Kelvin ivi ni kweli unahubiri kwa ajili ya kutangaza neno la mungu au kwa ajili ya kujipatia pesa!?" Nilimuuliza sababu bado sikuona kama Cyborg kaamua kuokoka kutokana na baadhi ya matendo yake yaliyokuwa yakijionyesha. Cyborg alinisogelea karibu na kuniambia. "Wewe unajua kabisa mimi ni
No comments:
Post a Comment