
PENZI LA MHALIFU 20 Afande Neema aliyekuwa amesimama karibu yangu alinisogelea nakuniongelesha kwa sauti ya chini. "Angel ivi ni masikio yangu au!!? yani leo mkuu anaitwa mke tena na kijana wa mtaani?" "Nyamaza kwanza Afande Neema tutaongea baadae" ilibidi nimwambie baada ya kumwona mkuu akisogea sehemu tulipo sisi pamoja na asikari waliokuwa wamemshika kijana aliyekuwa akiendelea kumuita mkuu wetu mke wake. Mkuu alifika na kuchomoa bastora, alimnyooshea kijana akitaka kumpiga risasi ila Afande Davi aliyekuwa karibu nae alimshika na kumzuia. Mkuu wetu alitaka kwenda kinyume na taratibu za nchi jinsi zilivyo ndiyo sababu iliyomfanya Afande Davi amzuie. "Mkuu acha usifanye
No comments:
Post a Comment