
PENZI LA MHALIFU 08 Nilifika na kuwakuta wenzangu wakinisubiri hivyo niliingia kwenye gari na kimbembe kilikuwa kwangu kwani siti zote zilikuwa zimekaliwa na watu kasolo siti moja ambayo pembeni yake alikuwa amekaa Afande Davi. Niliamua kwenda kukaa kwenye siti hiyo na safari ilianza. Afande Davi alikuwa akinitazama na kuamua kuniongelesha kwa mara ya kwanza. "Cyborg anaendeleaje!?" "Mzima tu" nilimjibu na Afande Davi alikaa kimya na kukoswa neno jingine la kuniongelesha. Jamani kuna wanaume wana midomo mizito ya kuongelesha mademu sijui tatizo huwa nini tu ndivyo alivyokuwa Afande Davi, baada ya kukoswa maneno ya kuniongelesha alijifanya amelala na mimi sikutaka kujihangaisha
No comments:
Post a Comment