
NILIMDANGANYA MKE WANGU NIMEFUKUZWA KAZI KUMBE NNALIKIZO MIEZI 3 Sehemu ya 04&05 Nilikaa kule chooni nilijihisi kuharisha ila sikuwa na haja kubwa, Nilikaa kwenye sinki la choo nikijiinamia huku nikijilaumu ,maana kama mke nikweli nampenda tena sio kidogo yaani nampenda sana tu , moyo uliniuma sana huku nikijiambia nimefanya kosa kubwa sana kumdanganya mke wangu , nikawaza labda nimwambie ukweli anaweza akatulia na mapenzi yakarudi kama zamani ,lakini upande mwingine nikawaza kuwa hata nikimwambia hawezi kubadilisha msimamo wake , nilikaa kule chooni nikaona mke wangu kanyamaza lakini kama anapilika pilika nyingine , nikaona ngoja nitoke nimuone anafanya nini , nikashangaa
No comments:
Post a Comment