
28--29 ENDELEA. ????NASEMA KWA MAMA Zilikuwa ni gari za polisi.... Waliingia Askari kama sita na kuwachukua akina Razac... Lidya alipewa karatasi fulani akaweka saini yake kisha kuwakabidhi... Naombeni nimkute Central Dar es Salam.. Aliongea Lidya akiwapa maagizo wale Askari... Nilikuwa kimya.... Wakati huo akina Razac na wenzie wanaondolewa mule ndani na Askari..... Tulitoka pia na kupanda gari la polisi hadi kwenye Lodge tulipowahi kurekodiwa na mama yake Dayana.. Tulimkuta Dada wa mapokezi ametulia tu anaangalia TV.. Lidya aliingia hadi kwenye chumba cha mapokezi na kumtoa.... Aliagiza Askari wampakie kwenye Gari pia..... Gari liliondolewa haraka lakini mimi na lidya tulibaki Moshi
No comments:
Post a Comment