
Hadithi NIMECHOKA Mume wangu alijiandaa haraka-haraka ili asichelewe kazini, nilimsaidia kuandaa vitu vidogo-vidogo muhimu kwake, ikiwemo saa na kidani cha mkononi alichopewa miaka mingi iliyopita na marehemu rafiki yake aliyeitwa Samson. Hivyo ndivyo alivyoniambia na alikuwa mwenye kukithamini sana. Aliharakisha kwasababu ilikuwa ghafla na dharula, haikuwa zamu yake kuingia kazini mchana kwasababu alitakiwa kuingia zamu ya usiku. Mume wangu alikuwa ni daktari wa hospitali binafsi, iliyokuwa mbali kidogo na nyumbani. Aliwaaga mapacha wetu Joanna na Joan, kwa kuwachezea vishavu vyao na wao kucheka maana walikuwa bado wadogo. Kwahiyo hawakuweza kuongea wakaeleweka, alikuja kunibusu paji langu la uso na kuondoka haraka.
No comments:
Post a Comment