
Franco ambaye alizaliwa Tarehe 6 Julai, 1938, katika Kijiji cha Sona Bata Magharibi ya Kongo, atakumbukwa na watanzania wakati alipofanya onyesho kweye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwaka 1973. Baba yake Joseph Emogo alikuwa mfanyakazi wa Shirika la reli wakati mama yake alikuwa mama wa nyumbani akioka mikate na kuuza Sokoni wakati akiwa bado mdogo wazazi wake walihamia katika Jiji la Kinshasa. Franco alipofikisha umri wa miaka Saba alitengeneza gitaa la kienyeji ambalo alilitumia kupiga na akiwavutia wateja pembeni mwa mama yake wakati akiuza mikate. Kipaji chake kiligunduliwa na mpiga gita Paul Ebengo Dewayon ambaye alijitolea kumfunza Franco
No comments:
Post a Comment