
DO YOU LOVE ME..... S2 (16) AM I WRONG? "Kuna nini...?" Nilimuuliza Rely ambaye alikuwa na hasira sio poa. Akanitazama usoni, macho yetu yalipokutana nilihisi utfauti katika macho yake. Kulikuwa na majimaji ambayo yalianza kudondoka. Ni machozi, nahisi Rely alikuwa na maumivu ambayo yalikuwa yakimuandama ndani ya mwili wake. Kulikuwa na kitu kinachomuumiza. Tukajikuta tunatizamana kwa zaidi ya dakika mbili, akaniuliza. "Unachokifanya unadhani ni kizuri?” “Sijaona ubaya” nilimjibu kwa dharau, kilio cha kwikwi kikazaliwa. Rely alianza kulia akisema “Inamaana unamhangaikia Rola si ndio? Hukumbuki kama alikufukuza kwake? Hakutaka tena mazoea na wewe? Hukumbuki?" “Yote tisa, hakuna kitu kitatafuta upendo wangu
No comments:
Post a Comment