
DO YOU LOVE ME 17 (S2) NO, I AM NOT WRONG Kabla ya kujibu kile nilichoulizwa, nilijifikiria kwa muda mrefu sana. Nikajibu. “Hapana” Jibu langu nikadhani huenda lingemstua sana Rely lakini hakuwa na wasiwasi wowote. Alijilaza kitandani. Nikastuka! Kwanini aulize halafu nimjibu na kulala pasipo hata kuendeleza maongezi? Sikupata jibu. Nami ilinibidi nijilaze. Nikawa ni mwenye mawazo mno hata usingizi haukuja vizuri. Usiku huu hatukuongeleshana lolote hadi palipokucha. Asubuhi iliyokuwa na baraka ilitia timu. Rely akawa wa kwanza kuamka, akaandaa chai na kuniletea kitandani. Hapa napo nilistuka. Inakuaje hadi ananiletea chai ikiwa hatuna maelewano mazuri? Anataka kuniua? Sikujipa majibu sahihi
No comments:
Post a Comment