
DO YOU LOVE ME 06 (S2) SAD MOMENT Niliingia mtaani kumtafuta Mama Rely kwa zaidi ya masaa 12 lakini sikuweza kumpata. Nilirudi nyumbani majira ya saa nne usiku nikiwa hoi bin taabani. Nikapoteza nguvu na akili ikafubaha sababu yule aliyesababisha hadi mwanamke huyu kupotea ni sehemu ya maisha yangu (Mama) kwahiyo mimi ndio nilipaswa kuwajibika mwanzo mwisho. "Enh! Umemuona mume wangu?" Aliniuliza Rely kwa sauti ya upole iliyojaa kitetemeshi. "Sijafanikiwa lakini kesho nitaenda tena" "Hakuna ambaye alikuambia kuwa amepatikana?" "Hakuna ila usijali" Nilimpatia moyo. Asubuhi ilipopambazuka, sikuwa na muda wa kupiteza kabisa. Jambo la kwanza lilikuwa ni kwenda katika masoko
No comments:
Post a Comment