
AIBU YA KUCHELEWA KUOLEWA ILINIFANYA NIKAOLEWA NA JINI ???????? Sehemu ya Nne ( 4 ) ************* @Kila Mtu ???????????????????????????????????????????????? ..Kinyonge nilifuta machozi na kuinuka nikitaka kwenda chumbani ila msichana wangu wa kazi alikuja na kusimama mbele yangu huku akiwa na glas ya maji. Nilimuangalia na kumtaka anipishe nipite akanambia " samahani dada naweza kuongea na wewe?" "Hapana Zubeda sio sasa, kama kuna lolote unalo hitaji tumia pesa yako nitakurudishia kesho na usinihesabie chakula" "Sihitaji pesa ila nataka kuongea na wewe kuhusu wewe mwenyewe "Kauli yake ilinishtua nikamuuliza "kuhusu mimi ukimaanisha nini?" "Kama hutojali naomba ukae samahani lakini" Nilimuangalia bila kusema
No comments:
Post a Comment