
PENZI LA MAFIA NA DOCTOR DYNESS ???????????????????????? BY DIANA STORIES Wtsp 0768328909 SEHEMU YA KWANZA(01) Katika hospital kubwa ya kifahali inayojulikana kwa jina la Aghakhan, kulionekana msafara wa magari ukiwasili eneo lile na kushuka vijana waliovalia suti nyeusi uku wengine wakiingia ndani ya hospital kwa ajili ya kwenda kuita madokta waje kusaidia kumchukua mgonjwa wao. Baada ya dakika kadhaa madokta baadhi waliwasili eneo lile na kwenda kumchukua mgonjwa aliyeletwa na ule msafara na moja kwa moja kumpeleka kwenye chumba cha matibabu. Baada ya mgonjwa kufikishwa eneo husika, wale vijana walio valia suti nyeusi walikutana kwa pamoja na kuanza kupewa maelekezo
No comments:
Post a Comment