
HAKI YANGU Na Layman Donsue mtunzi... Sehemu ya Kwanza Jua lilikuwa linaelekea kupotea machoni mwa dunia, anga likiwa limetawaliwa na rangi ya machungwa iliyochanganyika na vumbi la kijijini. Neema alisimama kando ya barabara ya changarawe, akiwa amebeba begi lake moja la mgongoni na mkoba wa mkononi. Safari kutoka Dar es Salaam hadi kijiji cha Kaselya huko Iringa ilikuwa ndefu na yenye uchovu, lakini kwa Neema, ilikuwa safari yenye matumaini makubwa. Alikuwa amerudi nyumbani baada ya miaka minne ya masomo chuoni, akiwa na shahada ya sheria mkononi na ndoto za kusaidia familia yake kuinuka kutoka maisha ya kawaida ya kijijini. Neema
No comments:
Post a Comment