
PENZI LA MHALIFU 02 Nilichukua kitambaa changu nakufunga jeraha langu nakuelekea walipo wenzangu. tuliwafikisha kituoni vijana tuliowakamata nakuanza kuwahoji ni wapi walipokuwa wakizitoa bangi na nani anayewauzia bangi pamoja na madawa ya kulevya. Tuliamua kutumia nguvu kwa kuwapiga mpaka walianza kusema wenyewe ni nani anayewauzia bangi. "Kila mtu huwa ana sehemu yake ya kununua bangi kwangu mimi huwa na nunua kwa Cyborg" "Emu rudia umesema huwa unanunua bangi kwa nani!?" Afande Davi alimuuliza kijana aliyesema kuwa huwa ananunua bangi kwa mme wangu. "Kwa Cyborg Afande" Kijana hiyo alimjibu na Afande Davi alinigeukia nakuniambia. "Mme wako anauza bangi nenda kamkamate mwenyewe
No comments:
Post a Comment